KINSHASA : Ajali ya ndege yauwa 38 | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Ajali ya ndege yauwa 38

Takriban watu 38 wamekufa wakati ndege ya mizigo iliotengenezwa Urusi ilipoanguka na kuripuka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Kinshasa.

Watu wengine 30 wamejerubiwa wakati ndege hiyo aina ya Antonov 26 inayoendeshwa na shirika la ndege la Congo Afrika One ilipoangukia nyumba muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa karibu wa kimataifa wa Ndjili.

Maiti zinaendelea kutafutwa kwenye vifusi na idadi ya vifo yumkini ikaongezeka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com