Kinana azungumzia ushindi wa CCM 2010 | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 08.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Kinana azungumzia ushindi wa CCM 2010

Kampeni za uchaguzi wa urais na ubunge utakaofanyika nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, ziko mbioni, ambapo wagombea wanaizunguka nchi nzima kuomba kura za Watanzania

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete

Mtetezi wa urais wa chama kinachotawala, Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, anaitembelea mikoa kadhaa ya nchi hiyo kuomba ridhaa za wananchi wakipe tena chama chake nafasi ya kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine mitano ijayo. Kikwete ndiye rais wa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, taifa linalotajwa kama kisiwa cha amani katika Afrika, na sasa anaomba tena nafasi hii kwa mara ya pili.

Katika mahojiano haya, Othman Miraji anaongea na Mkurugenzi wa Kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana, anayezungumzia muelekeo wa mambo kwa upande wao.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com