1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Mahasen chafika kusini mwa Pwani ya Bangladesh

MjahidA16 Mei 2013

Kimbunga Mahasen leo kimelipiga eneo la kusini mwa pwani ya Bangladesh kwa mvua kubwa na upepo mkali, hali iliosababisha zaidi ya watu milioni moja kuhamishwa kutoka eneo hilo.

https://p.dw.com/p/18Z2l
Kimbunga Mahasen
Kimbunga MahasenPicha: picture-alliance/AP Photo

Kulingana na Mohammed Shah Alam mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa ya Bangladesh, kimbuka hicho kilikumba eneo hilo hii leo asubuhi na atahri zake kuanza kuonekana mara moja. Tayari watu wanne wameuwawa, mmoja anasemekana kuzama majini na mwengine kuangukia na mti uliokuwa karibu.

Kabla ya kimbunga hicho kupiga eneo la kusini mwa nchi hiyo tayari vifo 18 vilivyofungamanishwa na kimbunga Mahasen viliripotiwa Bangladesh, Myanmar na Sri Lanka.

Hata hivyo maafisa wa idara ya hali ya hewa wanasema Kimbunga hicho kilichokumba mji wa Sitakundu, karibu na mji wa Chittagong nchini Bangladesh kinaendelea kusonga mbele katika wilaya ya watalii ya Cox's Bazaar, lakini hofu yake ya kusababisha maafa zaidi katika maeneo hayo imeondolewa kutokana na Kimbunga Mahasen kupoteza nguvu zake.

Mwanamke anayetumia anayejikinga na mvua kutokana na kimbunga Mahasen
Mwanamke anayetumia anayejikinga na mvua kutokana na kimbunga MahasenPicha: Reuters

Kwa upande wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na maswala ya misaada ya kibinaadamu imesema kwa sasa kunaweza kupatikana magonjwa ambayo yanaweza kuwa na hatari kubwa katika maisha ya binaadamu kwa watu milioni 8.2 nchini Bangladesh, Myanmmar na Kaskazini Mashariki mwa India.

Hata hivyo hatari kubwa imejitokeza kwa maelfu ya watu waliokosa makaazi wanaoishi katika makambi ya plastiki kwenye kambi za wakimbizi karibu na Magharibi mwa pwani ya Myanmmar.

Kimbunga kitachukua siku moja kupita Bangladesh

Baada ya kuondolewa katika makaazi yao kutokana na ghasia za kikabila, wakimbizi hao wanaotoka katika jamii kubwa ya waislamu walikataa kuondolewa katika kambi zao kwa sababu ya kukosa imani na baadhi ya maafisa katika nchi iliyojaa jamii ya wa Buda ambako jamii ya Rohingya imekuwa ikibaguliwa kwa miongo mingi.

Hadi sasa takriban wa Rohingya 50 hawajulikani waliko kufuatia boti yao kuzama wakati walipokuwa wanakimbia kimbunga Mahasen.

Ferry zinazotumika kusafirisha watu kutoka ngambo moja hadi nyengine pamoja na huduma za boti zote zimesimamishwa na hata mashirika mengine katika eneo hilo kufungwa. Jeshi la Bangladesh limesema limeweka tayari meli 22 na helikopta 19 za kijeshi kupambana na hali halisi.

Kambi ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa
Kambi ya wakimbizi ya Umoja wa MataifaPicha: Soe Than Win/AFP/Getty Images

Kimbunga Mahasen kinasemekana kupita pole pole na kukadiriwa kuwa inaweza kuchukua siku moja nzima kupita katika pwani ya Bangladesh.

Mkuu wa serikali za mitaa katika wilaya ya Cox's Bazar, Ruhul Amin ametumia jengo lake la ghorofa 4 kuwahifadhi karibu watu 400 wakati kukishuhudiwa mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo.

Mwandishi: Amina Abubakar/AP/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman