1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha umoja wa mataifa kitasalia kwa miezi sita zaidi Golan

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiq

New-York:

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limeunga mkono kwa sauti moja, kikosi cha wachunguzi wa kimataifa kisalie kwa miezi sita zaidi katika milima ya Golan.Wachunguzi hao wa Umoja wa mataifa wamekua wakisimamia eneo linalowatenganisha wasyria na waisrael katika milima hiyo ya Golan tangu miaka 32 iliyopita.Kikosi hicho kina wanajeshi 1025 wa kutoka Austria,Canada,India,Japan,Nepal,Poland na Slovakia.