Kikao cha tisa cha Bunge kufunguliwa leo | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Kikao cha tisa cha Bunge kufunguliwa leo

Je wabunge wataidhinisha kuwa sheria muswaada juu ya kuunda serikali ya mseto?

Baada ya mwafaka kufikiwa juu ya mzozo wa ksiasa leo bunge lafunguliwa'

Baada ya mwafaka kufikiwa juu ya mzozo wa ksiasa leo bunge lafunguliwa'

NAIROBI

Rais Mwai Kibaki leo anatarajiwa kufungua rasmi kikao cha tisa cha bunge na kufungua ukurasa mpya baada ya mazungumzo yaliyofikia makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto.Hotuba ya rais Kibaki inatarajiwa kuelezea miongoni mwa mambo mengine sera ambazo zitatoa muongozo wa jinsi serikali hiyo mpya itakavyokuwa.

Hapo jana Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi kutawanya maandamano yaliyokuwa yakifanywa na vija awa kundi haramu la Mungiki katika mji mkuu Nairobi.Waandamanji hao walikuwa wakidai kuachiliwa huru kutoka jela kiongozi wa kundi hilo ambalo linadaiwa kuendesha mauaji mengi nchini humo.

Kwengineko Umoja wa Mataifa umenzisha kundi maalum la wataalamu ambao watakuwa tayari kwa ajili ya kuusadia umoja huo kukabiliana na mizozo ulimwenguni kama sehemu ya harakati za kufanikisha juhudi za usuluhishi katika nchi zenye mizozo.Kundi hilo maalum lenye wanacham watano ambalo liliwatuma wanachama wake wawili wiki hii nchini Kenya litahusika katika kuwasaidia wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanaopewa kazi ya kutatua mizozo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com