1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali.Rwanda yamrejesha nyumbani balozi wake kutoka Ufaransa.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpo

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Rwanda Charles Murigande amesema wamemtaka balozi wao nchini Ufaransa arejee nyumbani.

Rwanda imeashiria uwezekano wa kuvunjika uhusiano pamoja na Paris kutokana na mvutano uliosababishwa na waranti zilizotolewazo.

Hayo yanafuatia Jaji wa Ufaransa kutoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa maafisa tisaa wa Rwanda wanaotuhumiwa kuwa nyuma ya mauaji ya mwaka 1994 katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Maafisa hao tisaa wanasemekana kuwa karibu sana na Rais Paul Kagame ambae jaji huyo anasema ndie aliyeviamrisha vikosi vya RPF kuidungua ndege aliyokuwa akisafiria Rais iliyokuwa ikiendeshwa na rubani wa Kifaransa.

Shambulio hilo ndilo lililozusha mauaji ya halaiki ya malaki ya Watutsi na wa Hutu wenye misimamo ya wastani.

Rais Kagame amekanusha madai ya jaji Jean-Louis Bruguiere akisema madai hayo yamechochewa kisiasa.