1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Kudunguliwa kwa ndege ya Habyarimana kuchunguzwa

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gg

Rwanda imeanzisha tume ya uchunguzi wa kudunguliwa kwa ndege iliokua imemchukuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Juvenal Habyaraimana tukio ambalo linaonekana kuchochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo takriban watu 800,000 waliuwawa.

Waziri wa habari Laurent Nkusi ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters bila ya kufafanuwa kwamba baraza la mawaziri limetangaza watu wa kuunda tume huru ya kutafuta ukweli.

Suala hilo lilisababisha mvutano wa kidiplomasia na Ufaransa mwaka jana baada ya hakimu mmoja wa Ufaransa kutaka Rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame ashtakiwe kwa kifo cha Habyarimana.

Kagame ambaye wakati huo alikuwa ni kiongozi wa waasi amekanusha kuhusika kwa njia yoyote ile na kuangushwa kwa ndege hiyo.