1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev.Mawaziri wapeleka barua za kujiuzulu kwa rais.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1G

Mawaziri watano wa Ukraine kutoka katika chama cha Rais Viktor Yushchenko, wamewasilisha hati za kuacha kazi, baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo yenye nia ya kubuni njia za kuunda serekali ya umjoa na vyama vinavyounga mkoro Urusi kushindwa.

Mawaziri hao watano ni kutoka katika wizara ya Sheria, Afya, Kilimo, Vijana na Mambo ya ndani.

Hata hivyo chama cha Rais Yushchenko kijulikanacho kama Our Ukraine Party, kwa hivi sasa kina wingi wa robo tatu ya wingi wa viti Bungeni, na kimeendelea kukataa kushiriki katika kuunda serikali ya muungano wa vyama vinne.