KIEV: Viongozi wa Ukraine wajaribu kumaliza ugomvi wao | Habari za Ulimwengu | DW | 26.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV: Viongozi wa Ukraine wajaribu kumaliza ugomvi wao

Rais Viktor Yushchenko na Waziri Mkuu Viktor Yanukovich wa Ukraine wanakutana katika mji mkuu Kiev.Azma ya majadiliano hayo ni kutenzua mgogoro wa kisiasa kati ya viongozi hao wawili.Mvutano wa kinyanganyiro cha madaraka,ulifikia upeo wake siku ya Ijumaa,baada ya rais kutoa amri ya kupelekwa vikosi zaidi vya jeshi la wizara ya ndani,mjini Kiev.Amri hiyo ilikwenda kinyume na matakwa ya waziri wa ndani Vasyl Tsushko.Ripoti zinasema,maelfu ya wanajeshi wapo njiani kwenda mji mkuu Kiev.Viongozi hao wawili wanatazamiwa pia kujadili tarehe ya kuitisha uchaguzi wa bunge.Mwezi uliopita Yushchenko alitoa amri za kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi kabla ya wakati wake.Sasa Yanukovich amekubaliana na uchaguzi wa mapema,lakini amesema hauwezi kufanywa kabla ya majira ya mapukutiko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com