1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Rais Putin ziarani Ukraine

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChC
Rais Hugo Chavez wa Venezuela
Rais Hugo Chavez wa VenezuelaPicha: AP

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, amewasili leo nchini Ukraine kwa ziara ya siku moja, huku juhudi za ikulu ya Kremlin kuboresha udhibiti wa taifa hilo zikiendelea kufaulu. Rais Putin atakutana na rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko, na mawaziri wanaoongozwa na waziri mkuu wa Ukraine, Viktor Yanukovic.

Ziara ya Putin ni ya kwanza tangu Viktor Yanukovic aliporudi madarakani baada ya chama chake kushinda uchaguzi wa bunge mnamo mwezi Machi mwaka huu. Katika mazungumzo ya leo, Ukraine inatarajiwa kuishinikiza Urusi iondoe jeshi lake la wanamaji katika bahari nyeusi.