Kibaki aridhia serikali ya Umoja wa Taifa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 05.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Kibaki aridhia serikali ya Umoja wa Taifa

---

NAIROBI:

Taarifa kutoka Nairobi, zasema rais Mwai Kibaki wa Kenya, yutayari kuunda serikali ya Umoja wa Taifa ili kumaliza ugomvi na machafuko yaliofuatia uchaguzi.Rais Kibaki amesema pia yuko tayari kuchangia zaidi kurejesha suiluhu na kuponesha m,ajaraha yaliozuka nchini Kenya.Taarifa kutoka Idara ya habari ya rais iliotolewa baada ya mkutano wake na waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani Jendayi Frazer ilisema.

Bibi Jendayi Frazer alikutana hapo kabla leo na Kiongozi wa upinzani Bw.Raila Odinga kuhimiza suluhisho la amani kufuatia uchaguzi wa rais uliozusha machafuko makubwa kwa siku kadhaa nchini Kenya. Bibi Frazer alimpongeza rais Kibaki kwa kuonyoshea upinzani mkono wa suluhu ili kukomesha ghasia nchini Kenya .Alizitaka pande zote kuridhia mazungumzo kam,a njia pekee ya kujitoa kutoka msukosuko ulioikumba Kenya.

Chama cha upinzani cha ODM kinashikilia bado kuwa rais Kibaki ajiuzulu,Tume ya kimataifa ipatanishe na utawala wa mpito na sio serikali ya Umoja wa Taifa iundwe kabla uchaguzi mpya kuitishwa mnamo muda wa miez 3.

Hapo awali mshindi wa zawadi ya Nobel Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini aliekutana na pande zote mbili-alisema baada ya kukutana na rais Kibaki :

„Rais Kibaki haoneshi kukataa kabisa kuundwa kwa serikali ya muungano ila pakubalike tu kuna chombo cha utawala nchini.“

Msukosuko wa uchaguzi wa Kenya, ulizusha fadhaha kubwa kwa wakenya wanaoishi nchi za nje:

Kikundi cha waaandamanaji kiliandamana jana mbele ya Makao Makuu ya UM mjini New York,Marekani kikibeba biramu linalosema:KIBAKI-MUGABE-AMIN“ na „KENYA ISIGEUZWE RWANDA“.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com