1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibaki amualika Raila kwenye meza ya mazungumzo

8 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cljl

NAIROBI

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amemualika kwenye meza ya mazungumzo ya ana kwa ana kiongozi wa upinzani Raila Odinga kujadili maridhiano ya kitaifa baada ya uchaguzi uliozusha hali ya taharuki nchini humo.Endapo bwana Raila Odinga takubaliana na wito huo mazungumzo yatafanyika ijumaa ijayo.

Juhudi za kimataifa za kutafuta suluhu katika mzozo huo wa kisiasa zimepamba moto ambapo mjumbe maalum wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Jendayi Frazer alikutana na bwana Odinga hapo jana huku mwenyekiti wa Umoja wa Afrika John Kufour akitazamiwa kuwasili Kenya hii leo.Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na bwana Raiala Odinga mjumbe wa Marekani Jendayi Frazer alikubali kwamba wakenya wamedanganywa na viongozi walioko madarakani pamoja na taasisi husika katika uchaguzi ulipita akisema

Wakati huohuo shughuli za kugawa misaada kwa maelfu ya watu walioathirika na machafuko nchini humo zinaendelea.Zaidi ya watu 500 waliuwawa katika ghasia za kisiasa na wengine zaidi ya laki mbili wameachwa bila makaazi na wanaishi kwenye makambi nchini humo.