1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Serikali ya Sudan yapinga mahakama ya kimataifa ya uhalifu

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO1

Serikali ya Sudan imesema haitotambua uhalali wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ambayo hapo jana iliwataja watuhumiwa wawili wanaohusishwa na uhalifu wa vita katika jimbo la Darfur.

Mshataki mkuu wa mahakama hiyo ya mjini The Hague Luis Moreno Ocampo aliwataja watuhumiwa hao kuwa waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Sudan Ahmad Mohammed Harun na kiongozi wa wanamgambo wenye asili ya kiarabu wa Janjaweed Ali Kushayb.

Wawili hao wanatuhumiwa kwa kuhusika na makosa ya uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na ubakaji,mauaji,utesaji na madhila mengine dhidi ya binadamu katika jimbo hilo la mgogoro la Darfur.

Ocampo amesema kwamba uchunguzi juu ya uhalifu katika jimbo hilo bado unaendelea.Kwa upande wake serikali ya Sudan imesema mahakama hiyo haina haki ya kisheria ya kuwashtaki raia wa nchi yake na kwamba Sudan itamshataki mtuhumiwa yoyote wa uhalifu katika jimbo hilo.