KHARTOUM:Rais al Bashir na Salva Kiir washinda kuafikiana | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM:Rais al Bashir na Salva Kiir washinda kuafikiana

Rais wa Sudan Omar al Bashir na makamu wa rais wa Kusini mwa Sudan Salva Kiir wameshuindwa kufikia makubaliano katika mkutano wao wa jana.Mkutano huo uliodumu kwa muda mrefu ni wa kwanza kufanyika tangu wabunge wa eneo la kusini mwa Sudan kujiondoa serikali wiki jana.Rais Bashiri alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ikiwa ni juhudi za kutimiza madai ya wabunge wa eneo la kusini.Wabunge hao bado wanakataa kurejea serikalini ila wametoa ahadi ya kuendelea kudumisha makubaliano ya amani ya mwkaa 2005 yaliyomaliza vita vya wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21.

Kulingana na msemaji wa rais Mahjub Fadul hatua ya kuapishwa rasmi kwa baraza hilo jipya la mawaziri imeahirishwa hadi makubaliano kamili yatakapofikiwa aidha baadhi ya wabunge wamesafiri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com