Khartoum.Muungano wa mahakama za kiislamu wakataa mazungumzo. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum.Muungano wa mahakama za kiislamu wakataa mazungumzo.

Muungano wa mahakama za kiislamu wenye nguvu nchini Somalia hii leo umekataa kushiriki katika mazungumzo ya amani pamoja na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Viongozi wa kiislamu mjini Mogadishu wamesema kwamba mazungumzo hayawezi kuendelea hadi vikosi vya kijeshi vya Umoja wa Ulaya vitakapoondoshwa nchini Somalia na hadi Kenya itakapojumuishwa kama mpatanishi mwenza katika mazungumzo hayo.

Ujumbe wa waislamu ukizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP wamesisitiza msimamo wao wa kutoshiriki mazungumzo hayo hadi matakwa yao mawili yatakapotimizwa.

Nao ujumbe wa serikali ya Somalia uliowasili Khartoum tangu jana umesema kuwa, hautakubali masharti yaliyotolewa na upande wa pili, jambo ambalo bado linazusha khofu ya kuendelea na vita katika nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com