1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Serikali yatia saini makubaliano ya amani na waasi.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2h

Serikali ya Sudan imetia saini makubaliano ya amani na kundi la waasi kutoka mashariki mwa nchi hiyo.

Makubaliano hayo yana lengo la kumaliza mzozo uliodumu kwa muda wa miaka 12 baina ya pande hizo mbili.

Utiaji saini huo ulifanyika katika mji wa Asmara, mji mkuu wa Eritrea nchi ambayo imesaidia katika kupata makubaliano hayo ambayo ni pamoja na mgawano wa madaraka pamoja na utaratibu wa kiusalama kwa ajili ya jimbo hilo la mashariki mwa Sudan.

Makubaliano hayo ni ya tatu ya amani kutiwa saini na serikali ya Khartoum pamoja na makundi ya waasi katika maeneo kadha ya nchi hiyo kubwa ya Afrika katika muda wa miaka miwili.

Makubaliano kati ya Khartoum na kundi kubwa la waasi katika jimbo la Darfur yalitiwa saini mwezi May mwaka huu lakini yameshindwa kuendelea.