KHARTOUM : Serikali yashutumu ziara ya Kiir Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Serikali yashutumu ziara ya Kiir Marekani

Serikali ya Sudan leo hii imemshutumu vikali kiongozi wa kusini mwa Sudan Salva Kiir juu ya ziara yake ya Marekani na hiyo kuzidi kuutia makali mzozo wa kisiasa unaotishia amani ya miaka mwili kati ya kaskazini na kusini ya Sudan.

Kiir kiongozi wa utawala wa ndani kusini mwa Sudan na makamo wa kwanza wa rais wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Sudan ziara yake imerefushwa mjini Washington ili aweze kukutana na Rais George W. Bush.

Ziara yake hakifurahiwa na serikali ya Khartoum kwa kuonekana kuwa ni ishara ya serikali ya kusini mwa Sudan inaungwa mkono na Marekani baada ya Kiir kuwaondowa mawaziri wake kutoka serikali ya umoja wa kitaifa hapo mwezi wa Septemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com