KHARTOUM : Mazungumzo ya Somalia yasambaratika | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Mazungumzo ya Somalia yasambaratika

Mazungumzo ya amani ya Somalia yenye lengo la kuiepusha nchi hiyo na vita kamili kati ya Uongozi wa Kiislam na serikali ya mpito ya nchi hiyo yamesambaratika na kuzusha hofu ya kuzuka kwa mzozo utakaolikumba eneo zima la Pembe ya Afrika.

Pande hizo mbili zimeshindwa kukutana ana kwa ana katika mazungumzo hayo ya siku tatu yaliodhaminiwa na Umoja wa Afrika Umoja wa Ulaya na Umoja wa Waarabu.

Mazungumuzo hayo yaliokuwa yaanze hapo Jumatatu katika mji mkuu wa Sudan yameshindwa kufanyika kabisa wakati uongozi wa Kiislam ukigoma kukutana na ujumbe wa serikali ya mpito venginevyo wanajeshi wa Ethiopia walioko Somalia wanaondolewa. Pia wamedai kuondolewa kwa Kenya kama msuluhishi wa pamoja katika mazungumzo hayo.

Wito wa uongozi huo kutaka iundwe tume ya kimataifa kuchunguza ukweli wa mambo nchini Somalia umekataliwa na serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com