1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Mazungumzo ya Somalia mashakani

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxc

Uongozi wa Kiislam wenye kupinga mamlaka ya serikali ya mpito nchini Somalia umesema usingendelea na duru ya tatu ya mazungumzo ya amani hapo jana venginevyo Ethiopia inaondowa wanajeshi wake kutoka katika nchi hiyo yenye machafuko.

Pande zote mbili zilikutana na wanadiplomasia katika nyakati tafauti katika mji mkuu wa Sudan Khartoum baada ya ujumbe wa serikali kuwasili mjini humo hapo jana.Uongozi huo wa Kiislam unasema hakutakuwepo na mazungumzo ya ana kwa ana.

Pia umepinga nchi jirani ya Kenya kushirikiana uenyekiti wa mazungumzo hayo na Umoja wa Waarabu kwa kusema kwamba Kenya ilikuwa imeunga mkono kutumwa kwa wanajeshi wa kigeni nchini Somalia.