Khartoum: 10 wauwawa katika mapiganoya risasi mjini Omdurman. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum: 10 wauwawa katika mapiganoya risasi mjini Omdurman.

Polisi wawili na wapiganaji wanane wa kundi la zamani la waasi wa Darfur –Sudan Liberation Movement (SLM) wanaripotiwa kuuwawa katika mapigano ya risasi karibu na mji mkuu wa Sudan - Khartoum. Waziri wa habari Zubeihr Beshir Taha alisema katika mkutano na waandishi habari uliotangazwa na televisheni ya nchi hiyo, kwamba polisi imeripoti kupoteza watu wawili katika mapigano hayo jana, akiwemo Luteni kanali , na wanane wameuwawa na saba kujeruhiwa upande wa SLM. Mapigano hayo yanasemekana yalianza baada ya raia mmoja kulifyatulia risasi kundi la wanachama wa SLM katika sehemu wanakoishi raia mjini Omdurman. SLM ilitilia saini mkataba wa amani na serikali uliodhaminiwa na umoja wa Afrika Mei mwaka jana, lakini kumekua na wasi wasi unaozidi juu ya utekelezaji wa makubaliano hayo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com