1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya 'wanamapinduzi' yasitishwa Guinea ya Ikweta

Mohammed Khelef
3 Aprili 2019

Watuhumiwa hao ambao walishikwa tangu tarehe 22 Machi wanakabiliwa na mashitaka ya uhaini na kujaribu kumuondosha mkuu wa nchi, Rais Theodore Obiang Nguema.

https://p.dw.com/p/3GAcH
Äquatorialguinea Präsident Teodoro Obiang
Picha: picture-alliance/dpa/S. Lecocq

Kesi inayowakabili zaidi ya watu 150 wanaoshukiwa kushiriki jaribio la mapinduzi la mwezi Disemba 2017 nchini Guinea ya Ikweta, iliahirishwa siku ya Jumanne (Aprili 3).

Wakili wa utetezi, Ponciano Mbomio Nvo, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba hawajui sababu ya kusitishwa kwa kesi hiyo.

Watuhumiwa hao ambao walishikwa tangu tarehe 22 Machi wanakabiliwa na mashitaka ya uhaini na kujaribu kumuondosha mkuu wa nchi, Rais Theodore Obiang Nguema.

Hukumu ya mashitaka yote mawili inaweza kuwa kifo. Mashitaka mengine wanayokabiliana nayo ni ugaidi na kumiliki silaha na risasi, ambayo pekee yanaweza kuwafungisha miaka 20 jela.

Mnamo mwezi Januari mwaka huu, serikali ilidai kupanguwa jaribio la mapinduzi lililoratibiwa na mamluki wa kigeni ambao mwezi mmoja nyuma walikuwa wamejaribu kumuangusha Rais Obiang.