1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Taylor wa Liberia yanza tena kusikizwa

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClPH

THE HAGUE:

Kesi ya uhalifu wa kivita inayomklabili rais wa zamani wa Liberia imeanza tena kusikizwa mjini The Hague.

Mtaalamu mmoja wa biashara ya kimataifa ya almasi ndie shahidi wa kwanza kutoa ushahidi wake katika kesi ambayo imecheleweshwa kwa kipindi cha miezi sita.Shahidi huyo ameliambia jopo la majaji watatu kuwa biashara ya almasi ndio iliotia moto vita nchini Sierra Leone.

Taylor anashtumiwa kuunga mkono kundi la waasi katika nchi jirani ya Sierra Leone ,ambao walitenda unyama kama vile kuwakata vichwa wahanga wao katika vita vya ndani vilivyodumu miaka 10.Miongoni mwa mashataka 11 yanayomkabili Taylor ni;mauaji,ubakaji, na pia kuwatumia watoto kama wapiganaji.

Taylor amekana makosa yote.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa hamu ya Taylor ya kupata dhahabu kutoka Sierra Leone ni mojawapo wa kichocheo cha kuhusika kwake katika vita vilivyomalizika mwaka wa 2002.