Kesi ya Ken Saro-Wiwa na Shell | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kesi ya Ken Saro-Wiwa na Shell

Kesi hiyo inaanza jumatano hii New York.

Mjini New York , Marekani,. inaanza leo hukumu dhidi ya kampuni la mafuta la ROYAL DUTCH SHELL likichunguzwa kwa kadiri gani, lilihusika na kunyongwa kwa mkereketwa wa haki za kiraia na muandishi maarufu wa Ken Saro-Wiwa.

Mkereketwa huyo wa haki za kiraia wa Nigeria, akidai mapto yanayotokana na utajiri wa mafuta katika eneo la Ogoni, Nile Delta, pia yawanufaishe wakaazi wa eneo hilo .Marehemu hakutumia nguvu katika kampeni zake hatahivyo,Ken Saro-Wiwa alinyongwa miaka 15 iliopita na utawala wa kijeshi wa Nigeria wa wakati ule.

Hali aliopigania Ken Saro-Wiwa kuibadilisha haikubadilika,kusema kweli ,imezidi kuwa mabaya:Ni ijumapili iliopita tu chama cha waasi cha Niger-Delta-MEND kwa ufupi,kilihujumu jukwaa moja la kuchimbia mafuta na kikatamngaza vita dhidi ya serikali ya Nigeria.

Tangu mwishoni mwa miaka ya 1950,Nigeria ikichimba mafuta katika hali mbaya za uchafuzi wa mazingira yake.Upinzani uliogonga vichwa vya habari ulimwenguni katika Niger-Delta huko Ogoni mwanzoni mwa miaka ya 1990.Kilele cha kampeni hiyo ni kunyongwa kwa muandishi vitabu na mkerteketwa wa haki za kiraia Ken Saro-Wiwa aliehukumiwa kifo na Mahkama ya kijeshi ya utawala wa kidiktea wa wanajeshi wa Nigeria, 1995.

Ken akipigana biila matumizi ya nguvu ,lakini kutokana na mkandamizo wa watawala

wa kijeshi wa Nigeria, kizazi kipya cha waogoni kikaamua kushika silaha.

Kwahivyo, Niger Delta,haikutulia tena tangu wakati huo na wakati kesi dhidi ya Kampuni la mafuta la Shell kuhusu kunyongwa kwa Ken Saro-Wiwa,inaanza leo mawazo aliohubiri mkereketwa Saro-Wiwa yanapaliliwa upya.

Pale Ken saro-wiwa na wenzake 8 waliponyongwa alfajiri ya Novemba 10,1995,vilio vya hasira na uchukivu vilisikika ulimwenguni kote.Utawala wa kijeshi wa Jamadari Abacha ,sio tu ulłijaribu kumfunga kinywa mkereketwa huyo Saro-Wiwa,bali pia wapiganaji wa haki za waogoni,mojawapo kati ya makabila 250 ya Nigeria. Ken saro-Wiwa alisema,

" Sikuridhika na hali ya mambo katika Ogoni.Na ingawa nilikuwa bado kijana ,ilinidhihirikia wazi ,Ogoni hainufaiki hata kidogo na pato la mafuta yake.Nikaanza kuandika juu ya hali hiyo.Nilijua kuwa masilahi yetu hayatiwi maanani na wenye nguvu."

Ken Saro-Wiwa, alilalamika kuwa bomba la mafuta la urefu wa kilomita alfu kadhaa lilichafua mazingira ya mwambao wa pwani ambao hapo kabla ukiwaneemesha wakaazi wake katika uvuvi na sasa umejaa sumu.Na sasa hata misitu inakufa,bali hata umasikini wa wakaazi wake umezidi.

Muandishi Ken saro-Wiwa,akajiunga mwanzoni mwa miaka ya 1990 na chama kilichojiita ( Movement of the Survival of the Ogoni People) chama kinachopigania kudumu kwa watu wa Ogoni.Ken Saro-Wiwa na wenzake wakanyongwa bila hata kufanyiwa hukumu ya haki.Baadae Hakimu alieendesha mashtaka yake alikuja kuungama kwamba alihomngwa .Sasa Mwanawe Ken saro-Wiwa jr. anataka kujua ni nani aliemhonga fedha ?

"Tuna uhakika kwamba, kampuni la mafuta la Shell lina mkono wake katika kuteswa watu na kunyangowa,katika kuviteketeza vijiji vyake na katika kuchafua ardhi ya rutba.Na hataka katika kutimuliwa kwa wakaazi wake wengi .Tunahisi kwamba kampuni la Shell liwajibike."

Kwahivyo, Ken Saro-Wiwa jr, amelishtaki kampuni la Shell kutenda uhalifu dhidi ya binadamu na ni azma yake kuthibitisha kwamba, kunyongwa kwa baba yake kuna kidole cha kampuni hilo kubwa la mafuta.Anataka kuthibitisha kuwa kampuni la Shell lioligharimie kutiwa nguvuni na kuandaa mipango yote.Na anatumai kwa jicho la hali ya mambo ilivyo leo katika Niger-Delta, baba yake mhanga alioutoa kwa Ogoni,haukuwa wa bure.

Mwandishi:Alexander Göbel/ZR/Ramadhan Ali

Mhariri: M.Abdul-rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com