Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta yaahirishwa | Matukio ya Afrika | DW | 24.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta yaahirishwa

Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi za Uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague-Uholanzi, imepitisha uamuzi hapo jana wa kuahirisha kikao cha ufunguzi wa kusikilizwa kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Hatua hiyo imechukuliwa na mahakama hiyo kufuatia ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda la kutaka muda zaidi wa kujipanga katika suala la mashahidi wake.Mahakama hiyo imesema badala yake siku hiyo ya Tarehe 5 Februari kutafanyika kikao maalum kitakachowahusisha washiriki wote wanaohusiana na kesi hiyo.kikao ambacho upande wa utetezi wa Uhuru Kenyatta unatarajiwa kutoa pendekezo la kutaka kesi hiyo ifutiliwe mbali.

Ili kufahamu ni vipi uamuzi huo wa ICC ulivyopokelewa nchini Kenya na waathirika wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008, Saumu Mwasimba amezungumza na Patrick Muchiri ambaye ni mwakilishi wa waathiriwa hao katika eneo la Bonde la Ufa. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hpo chini.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Abdulrahman Mohammed

Sauti na Vidio Kuhusu Mada