1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya kampuni ya ulinzi ya Blackwater yaendelea Washington

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz3

Mahaka ya Marekani inayochunguza kesi inayoikabili kampuni ya Blackwater Worldwide, imewasikiliza mashahidi huku walinzi wa kampuni hiyo wakishatakiwa kwa kupuuza amri na kuondoka vituoni mwao muda mfupi kabla kushiriki katika kisa cha kuwapiga risasi na kuwaua Wairaki 17 mjini Baghdad nchini Irak.

Mashtaka mapya yaliyowasilishwa wiki hii katika mahakama ya mjini Washington, yanailaumu kampuni ya Blacwater kwa kutowapima walinzi wake kubaini ikiwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu mwilini zinazoathri uwezo wao wa kupitisha uamuzi.

Msemaji wa kampuni ya Blackwater amesema walinzi wote hawaruhusiwi kutumia dawa za aina hiyo lakina hakutoa maelezo zaidi juu ya mashtaka mengine yaliyowasilishwa mahakamani.