Kenya yatoroka tena na dhahabu mita 3000 kuruka viunzi. | Michezo | DW | 19.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kenya yatoroka tena na dhahabu mita 3000 kuruka viunzi.

Leo ni final ya mita 800 na 1.500.

default

Steffi Nerius -medali ya dhahabu yake.

Siku ya 4 ya mashindano ya riadha ulimwenguni mjini Berlin, ilikuwa shangwe na shamra shamra kwa wajerumani ,wakenya , wajamaica, lakini pia, wa Marekani,kwani msichana wao wa asiili ya Jamyaica, Sanya Richards, mwishoe, alitoroka na medali ya dhahabu kutoka mashindano makuu ulmwenguni. Mkenya Ezekiel Kemboi,amelirejesha tena Kenya tajii la mita 3000 kuruka viunzi ambako wakenya wanadai ndio nyumbanii kwao.

Leo ni finali ya mita 800 wanawake ambamo bingwa wa dunia kutoka Kenya Jeneth Jepkosgei ana miadi na bingwa wa Afrika Kusini,Caster Semenya.

Ezekiel Kemboi,jana alisema imetosha kiila mara kumaliza wapl na jana alitimka mbio katiika fnalii ya mita 3000 kuruka vunzi na kutawazwa bingwa baada ya kuja wapili mara 3 zilizopta.Muda wake wa dakiika 8 na sek.00.43 ndio muda bora kabisa wa mashindano haya.Mwenzake Kipkemboi Metlong, alibidi kuridhika na medali ya fedha.Mfaransa Bouabdellah Tahri,alwanyima wakenya medali ya 3 ile ya shaba aslpompiku mfondoni Paul Koech.Kemboi alitawazwa bingwa wa Olimpik 2004,lakni katika mashindano ya riadha ya dunia hakufaulu hadii jana kuparama jukwaa la washindi na kupigiwa wimbo wa tafa wa Kenya.Bingwa wa olimpk na wa zamanii wa duniia Brimin Kipruto aliangukia nafas ya 7.

Fiinali ya jana ya mita 3000 kuruka viunzi iilgubikwa na kutolewa nje ya mashindano hayo mmorocco Jamal Chatb aliegunduliwa na madhamb ya Doping.

Kenya leo joni, natazamia medali yake nyengne ya dhahabu katiika fnali ya mita 800 wanawake ambamo bingwa wa dunia Jeneth Jepkosgeii anatazamia kuchuana na muafrka Kusn Caster semenya.Hatima ya bingwa wa Olmpik Jelimo kwa sasa haijulikani.Amekataa rufaa kwa chama cha riadha cha IAAF baada ya kuangushwa katika mbio kabla finali.

Marekanii ilishangiriia medali yake nyengine ya dhahabu katika mta 400 wasiichana.Sanya riichards baada ya kusubiri nae ktambo kirefu kutawazwa malkia wa mbio zake, jana siku yake ilwada Berln.Kwa muda wake wa sek.49, aliinyakua medali ya dhahabu akmuachiia Shericka wiilliams wa jamaca le ya fedha.

Ilikua vigelegele jana uwanjani kwa mashabiki wa Ujerumani,kwani baada ya medalii za fedha na shaba, usku wa jana Steffi Nerius alijpatia medali ya dhahabu kuhetimisha maisha yake ya riadha.Na hivi ndivyo alivyofuraha ushindi wake akipgiwa wimbo wa tafa n a kusema:

"Siju nieleze vipi.......Nilitumai nikiwastua wapinzanii wangu katiika jarbio la kwanza tu la kurusha mkuki kwa kuuvurumisha mbal sana, huenda nikafanikwa kushnda.Kuwa mbinu hi imefaniikwa ni ajabu kabisa-supa."

Joni ya leo, mbali na finali ya mita 800 wanawake, tutajionea pia changamoto ya finali ya mita 1.500 wanaume ambamo mkenya Augustine Kiprono na mwenzake Asbel Kiprop wanamuahidi bingwa wa dunia mzaliwa wa Kenya Bernard Lagat,kumvua taji.

Muandishi:Ramadhan Ali /DPAE

Mharri: Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com