Kenya yatawala mbio za mita 3,000 | Michezo | DW | 25.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kenya yatawala mbio za mita 3,000

Mwanariadha wa Kenya Ezekiel Kemboi ameipa Kenya medali ya pili ya dhahabu katika mashindano ya dunia yanayoendelea mjini Beijing, China. Kenya ilichukua nafasi nne za kwanza katika mbio za mita 3,000

Hilo ni taji la nne la mfululizo la Kemboi katika mashindano ya dunia baada ya kuwaongoza Wakenya wenzake kushinda nafasi za kwanza nne bora katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Conseslus Kipruto alichukua fedha, Brimin Kipruto akachukua shaba huku Jairus Kipchoge Birech akichukua nafasi ya nne

Mpinzani wao raia wa marekani Evan Jagger aliona kivumbi wakati Wakenya hao walipotimka mbio.

Awali mwanariadha wa Kenya Vivian Ceruiyot aliishindia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 10,000 kwa upande wa wanawake. Vivian alishinda medali za fedha katika mbio za mwaka 2003, 2005, 2007.

Mwanariadha wa Ethiopia Gelete Burka alichukua medali ya fedha baada ya kumaliza wa pili nyuma ya Cheruiyot. Medali ya shaba ilimwendea Mmarekani Emily Infield.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo