1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Wapinzani NASA kukutana na serikali?

16 Januari 2018

Viongozi wa muungano huo mkuu wa upinzani wako tayari kufanya mazungumzo na serikali ya Rais Kenyatta ila kwa masharti fulani. Viongozi hao walisema pia wako tayari kujadili suala la serikali ya pamoja.

https://p.dw.com/p/2quRE
Kiongozi wa upinzanu Kenya, Raila Odinga
Picha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

J2 16.01 Kenya/ NASA - MP3-Stereo

Bado viongozi hao wameshikilia msimamo wao wa kumuapisha Raila Odinga kama rais mbadala wa Kenya na Kalonzo Musyoka kama makamu wake wa rais, hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 31 Januari. Basi kwa mengi zaidi juu ya hili DW imezungumza na mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM kinachounda muungano wa upinzani NASA nchini Kenya, Philip Etale, anayeanza kwa kueleza masharti wanayoyataka yaangaziwe kabla ya kuwepo kwa majadiliano ni yepi.