1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Polisi wawakimbia maafisa wa kupambana na rushwa

Sekione Kitojo
29 Novemba 2018

Polisi nchini Kenya wamewasaidia wenzao wawili ambao walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za rushwa kutoroka.

https://p.dw.com/p/396zO
Kenia Wahlen Gewalt Einwohner unter Polizeischutz in Naivasha
Picha: AP

Polisi nchini Kenya wamewasaidia wenzao wawili ambao walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za rushwa kutoroka mahabusu  kwa kufyatua risasi za tahadhari kuwatisha maafisa wa kupambana na rushwa waliokuwa wakiwashikilia polisi hao.

Polisi hao wawili, ambao wanafanyakazi katika idara ya uchunguzi wa uhalifu, walikamatwa mjini Nairobi jana jioni katika  operesheni  iliyofanywa  na  maafisa  wa kupambana   na  rushwa  wakijaribu  kuwatega  kwa kutumia  hongo  ya  shilingi 100,000 za  Kenya.

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi  nchini  Kenya, EACC,  imesema  watuhumiwa  hao  wawili  walikamatwa na  kufungwa  pingu lakini  waliokolewa  na  wenzao kutoka  kituo  cha  polisi  cha Kabete  ambao walifyatua risasi  kadhaa hewani kama tahadhari  ili  kuwawezesha kutoroka.

Polisi hao waliokimbia na fedha hiyo mtego wakiwa wamefungwa pingu, bado wanatafutwa.