Kenya imewataka wanadiplomasia wa kigeni kutoingilia siasa wakati wa uchaguzi | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kenya imewataka wanadiplomasia wa kigeni kutoingilia siasa wakati wa uchaguzi

Serikali ya Kenya imewataka wanadiplomasia wa kigeni kukoma kuingilia siasa za ndani ya nchi hiyo inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Naibu waziri wa mambo ya nje nchini humo Moses Wetangula alitoa matamshi ya kuwaonya wanadiplomasia hao baada ya mwanadiplomasia wa Uingereza nchini Kenya Adam Wood kuitaka serikali kutowalazimisha wafanyikazi wa serikali kuipigia kura wakati wa uchaguzi.

Saumu Mwasimba alizungumza na Dkt.Noeh Wekesa ambaye ni waziri wa sayansi na technologia na vile vile rafiki wa karibu wa Bw. Wetangula.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com