Kenya: Ghasia zaibuka mjini Mombasa | Matukio ya Afrika | DW | 03.02.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kenya: Ghasia zaibuka mjini Mombasa

Zaidi ya washukiwa 100 wanatazamiwa kufikishwa mahakamani leo Mombasa kufuatia ghasia za umwagikaji wa damu zilizokumba sehemu za mji huo jana jioni huku Polisi ikiwa bado inasita kutoa idadi kamili ya watu waliouawa.

Ghasia zilizoibuka mjini Mombasa

Ghasia zilizoibuka mjini Mombasa

Watu watatu akiwemo afisa mmoja wa Polisi yahofiwa waliuwawa wakati wa ghasia hizo zilizozuka baada ya Polisi kuuvamia Msikiti mmoja na kuvunja kongamano la wafuasi wa dini ya Kiislamu,kwa madai kwamba kongamano hilo lililenga kuendeleza harakati za kundi la Alshabab.

Kutoka mjini Mombasa mwandishi wetu Eric Ponda ametukusanyia taarifa ifuatayo kuhusu hali ilivyo sasa. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Eric Ponda

Mhariri:Mohammed AbdulRahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada