Kenya: Bunge latupilia mbali ripoti kuhusu sukari ya magendo | Media Center | DW | 10.08.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Kenya: Bunge latupilia mbali ripoti kuhusu sukari ya magendo

Bunge la Kenya siku ya Alhamisi liliitupilia mbali ripoti kuhusu sukari iliyoingizwa nchini humo kimagendo na ambayo ilidaiwa kuwa na madini ya zabaki ambayo si salama kwa matumizi wa binadamu. Hatua hiyo imetajwa kuwa inaweza kuweka doa katika juhudi za serikali ya Kenya kupiga vita uagizwaji wa sukari kwa njia isiyo halali.

Sikiliza sauti 03:04

Bunge la Kenya jana liliitupilia mbali ripoti kuhusu sukari iliyoingizwa nchini humo kimagendo na ambayo ilidaiwa kuwa na madini ya zabaki ambayo si salama kwa matumizi wa binadamu. Hatua hiyo imetajwa kuwa inaweza kuweka doa katika juhudi za serikali ya Kenya kupiga vita uagizwaji wa sukari kwa njia isiyo halali.

Kukataliwa kwa ripoti hiyo aidha kumewasababishia hasara ya mamilioni ya pesa Wakenya, kwani takriban shilingi milioni kumi zilitumika kuwalipa wanachama thelathini na wanane wa kamati iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi kuhusu sukari hiyo.

Baadhi ya wabunge hata hivyo wameitaja hatua ya kutupiliwa mbali kwa ripoti hiyo kuwa ushindi kwa mawakala wa sukari, huku wakitilia shaka nanma mjadala kuhusu suala hilo ulivyoendeshwa.

Na ili kupata mtazamo kamili wa wakuu wa watumiaji bidhaa nchini Kenya, Sophia Chinyezi amemuhoji Mkuu wa Chama cha Kutetea Maslahi ya Wanunuzi nchini Kenya COFEK, Steven Mutoro, (pichani) na kwanza ameanza kwa kumuuliza tathmini yake kuhusu hatua hiyo.