KENNEBUNKPORT:Urusi na Marekani kuondoa tofauti zao | Habari za Ulimwengu | DW | 02.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KENNEBUNKPORT:Urusi na Marekani kuondoa tofauti zao

Rais wa Marekani George W Bush na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin waanendelea na mazungumzo yao yanayolenga kuondoa mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Hilo linasababishwa na baadhi ya matukio yakiwemo mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya Mashariki.

Hata hivyo pande zote mbili zilichelea kujadilia masuala maalum na badala yake kujaribu kuwa na maelewano katika mikutano itakayofuatia.Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa Rais Putin Sergei Prikhodko.

Rais Bush amekuwa akikosoa mfumo wa demokrasia nchini Urusi ambayo kwa sasa ina nguvu zaidi ya kuvutia upande wao katika ushirikiano na mataifa ya Ulaya na Marekani kufuatia ongezeko la pato lake kwasababu ya biashara ya nishati.

Urusi kwa upande wake haionyeshi ishara zozote za kubadili mtizamo wake katika suala kama mpango wa marekani wa kuweka makombora ya kujihami katika Jamhuri ya Czech na Poland.marekani inashikilia kuwa lengo lake ni kujihami na mataifa adui zake mfano Iran.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com