Kazi ya kutafuta miili ya wahanga kuanza tena Italia | NRS-Import | DW | 05.10.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Kazi ya kutafuta miili ya wahanga kuanza tena Italia

Idara ya huduma za dharura nchini Italia inatarajia kurejea kusaka miili ya watu waliofariki baharini leo(05.10.2013) licha ya hali mbaya ya hewa na mawimbi makubwa baada ya boti kuzama katika bahari ya Mediterranean.

A still image taken from video released on October 4, 2013 by the Italian Coastguard shows migrants rescued from the water off the southern Italian island of Lampedusa on Thursday October 3, 2013. Italian rescue workers have pulled 111 bodies from the migrant boat that sank off the island of Lampedusa on Thursday and expect to recover more than a hundred more from the submerged wreck, a coastguard official said on Friday. Footage taken October 3, 2013. REUTERS/Italian Coast Guard/Handout via Reuters (ITALY - Tags: DISASTER) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. MANDATORY CREDIT

Vyombo vya idara ya huduma za dharura ya Italia

Katika boti hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya abiria 450, idara ya huduma za dharura imethibitisha kuwa wahamiaji 111 kutoka Afrika wamefariki na kiasi wengine 200 bado hawajulikani waliko.

Wakati utafutaji wa miili nje ya kisiwa cha Lampedusa umesitishwa jana Ijumaa(04.10.2013) kutokana na hali mbaya ya hewa , kiongozi wa kanisa Katoliki ambaye alizungumza akionesha hisia kali amesema, kuwa "ilikuwa siku ya kububujikwa na machozi" katika "dunia hii ya kikatili" ambayo inawapuuza wakimbizi.

Serikali imeuomba umoja wa Ulaya usaidie kuzuwia uingiaji wa wahamiaji , wakati nchi hiyo inaomboleza vifo hivyo.

Pope Francis celebrates a mass during his visit at Lampedusa Island, southern Italy, July 8, 2013. Pope Francis makes his first official trip outside Rome on Monday with a visit to Lampedusa, the tiny island off Sicily that has been the first port of safety for untold thousands of migrants crossing by sea from North Africa to Europe. The choice of Lampedusa is a highly symbolic one for Francis, who has placed the poor at the centre of his papacy and called on the Church to return to its mission of serving them. REUTERS/Alessandro Bianchi (ITALY - Tags: RELIGION)

Papa Francis wa kanisa Katoliki

Wafanya maombi

Wakaazi wa kisiwa hicho kidogo cha jamii ya wavuvi wamefanya misa pamoja na maandamano ya kimya kimya ya kuwasha mienge , wakati bendera zikipepea nusu mlingoti nchini Italia jana Ijumaa na shule zilifanya kumbukumbu ya wahanga kwa kukaa kimya kwa dakika moja.

"Hii ni shughuli muhimu kwa wahanga na kwetu sisi", amesema Michele Rossi , mkaazi wa eneo hilo ambaye ni mmiliki wa duka. "Tumezowea kufanya kila tunaloweza kuokoa maisha lakini hatujaona kitu kama hiki."

Idara ya huduma za dharura katika kisiwa hicho , ambacho kiko katika eneo la mbali upande wa kusini kabisa mwa Italia , zimesema kuwa zimetoa kutoka majini miili 111 hadi sasa na wameokoa watu 155 ambao wako hai kutoka katika boti hiyo ambayo inakisiwa kuwa ilikuwa na watu kati ya 450 na 500.

Waokoaji wamesema mawimbi makubwa na upepo katika kisiwa hicho huenda yameisukuma miili mingine mbali zaidi ndani ya bahari lakini hawakuweza tena kuondoka bandarini kwasababu ya upepo mkali pamoja na mawimbi yenye urefu wa mita mbili.

epa03894672 Bodies retrieved from the sea are pictured inside a hangar in Lampedusa, Italy, 03 October 2013. A boat carrying about 500 people from North Africa caught fire before reaching the Italian island of Lampedusa on 03 October. Rescuers recovered 82 bodies and reported at least 250 people were still missing. EPA/FRANCO LANNINO +++(c) dpa - Bildfunk+++

Maiti za wahamiaji waliokufa maji

"Kuna hali ya kuogofya. Maiti kadha , huenda kwa mamia," Rocco Canell, ambaye anaendesha shule katika kisiwa hicho ya udereva na alikwenda katika eneo la bahari kabla ya msako kusitishwa , ameliambia shirika la habari la Italia ANSA.

"Miili imepandana, imelundikwa, mmoja juu ya mwingine. Wale wenye bahati ni wale waliofariki kwanza," amesema baada ya kutoka katika eneo hilo la kutisha lililopinduka boti hiyo, ambapo boti hiyo imezama kabisa katika kina cha karibu mita 40.

Wakiwa na hofu waliruka majini

Wahamiaji , karibu wote wakiwa ni Waeritrea , waliondoka kutoka bandari ya Libya ya misrata na walisimama kuchukua watu zaidi mjini Zuwara, pia nchini Libya.

Wamewaambia waokoaji kuwa walichoma blanketi katika boti hiyo nje kidogo ya Lampedusa kuashiria kwa walinzi wa pwani baada ya boti yao kuanza kuingiza maji.

Moto huo haraka ukasambaa katika boti hiyo yenye urefu wa mita 20, ambayo ilizama majira ya alfajiri siku ya Alhamis(03.10.2013) ikiwa ni mita chache tu kutoka Lampedusa, wakati abiria waliokuwa na hofu kubwa walianza kuruka majini wakiwa wamemwagikiwa na mafuta.

epa03894368 Italian rescue workers recover dead bodies from a boat at the port of Lampedusa, Italy, 03 October 2013. A boat packed with African migrants caught fire and sank off the southern Italian island of Lampedusa on 03 October. The bodies of 40 migrants have been found off Lampedusa, the Ansa news agency reported citing the coast guard, taking the death toll to at least 133. EPA/ETTORE FERRARI +++(c) dpa - Bildfunk+++

Miili ya wahamiaji katika kisiwa cha Lampedusa

Nahodha wa boti hiyo raia wa Tunisia , ambaye aliwahi kukamatwa na polisi nchini Italia mwezi Aprili kwa kusafirisha watu kinyume na sheria na kurejeshwa nchini mwake Tunisia , anashikiliwa na polisi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Italia Angelino Alfano ametoa wito wa kuongezwa msaada wa mataifa ya Ulaya katika kufanya doria katika mipaka ya majini nchini Italia pamoja na hatua zaidi katika nchi barani Afrika kuzuwia wimbi la wakimbizi wanaovuka mipaka na kuingia nchini humo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Amina Abubakar

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com