kazi kubwa yamsubiri Rouhani Iran | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

kazi kubwa yamsubiri Rouhani Iran

Wairan wanapenda maajabu. Taifa hilo linaishangaza jamii yake, na jamii inaushangaza uongozi na wote huishanza jamii ya kimataifa. Hufanya hivyo kila wakati, na hata hivi karibuni katika uchaguzi wa rais nchini humo.

epa03746243 Thousands of supporters of newly elected President Hassan Rowhani take part during a street festivities right after the official announcement of his victory, in Tehran, Iran, 15 June 2013. Reformist candidate Rowhani has won Iran's presidential election with more than 50 percent of votes, outclassing the other five candidates. After eight years of hardliner Mahmoud Ahmadinejad, the new president Rowhani is likely to bring about a real change in both domestic and foreign policy. EPA/ABEDIN TAHERKENAREH

Uchaguzi wa Iran 2013

Kwa mujibu wa baraza la ushauri nchini Iran karibu asilimia 99 ya wagombea wa uchaguzi waliondolewa na kuacha nafasi finyu ya kuweza kuleta mshangao, baada ya kubakia wagombea sita tu katika uchaguzi huo. Hassan Ruhani mwenye msimamo wa wastani pamoja na wagombea wengine watano wahafidhina waliingia katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania madaraka.

Hakuwapo mgombea ambaye ni maarufu miongoni mwa wahafidhina waliogombea uchaguzi huo , na Ruhani alikuwa hafahamiki sana. Kwa hiyo mtu angetarajia kuwa uchaguzi huo ungeingia katika duru ya pili, kwa kiasi kikubwa baina ya wagombea wawili wahafidhina. Na ghafla kila kitu kikaenda tofauti kabisa.

epa03746244 Thousands of supporters of newly elected President Hassan Rowhani take part during a street festivities right after the official announcement of his victory, in Tehran, Iran, 15 June 2013. Reformist Rowhani has won Iran's presidential election with more than 50 percent of votes, outclassing the other five candidates. After eight years of hardliner Mahmoud Ahmadinejad, the new president Rowhani is likely to bring about a real change in both domestic and foreign policy. EPA/ABEDIN TAHERKENAREH

Wairan wakishangiria ushindi wa Rouhani katika uchaguzi wa rais

Uchaguzi wa rais nchini Iran umeamuliwa katika duru ya kwanza tu.

Zoezi la kuhesabu kura

Zoezi la kuhesabu kura lilikawia kuliko ilivyopangwa. Shauku ilikuwa inapanda kila dakika, hadi pale wizara ya mambo ya ndani nchini Iran ilipotoa rasmi matokeo ya uchaguzi huo.

Hakuna mtu aliyefikiria kuwa Ruhani angepata ushindi mkubwa na usio na shaka namna hiyo.

Hali hii iliwezekanaje basi?

An Iranian woman holds her purple scarf, the campaign color of moderate presidential candidate Hassan Rowhani, as she celebrates along Valiasr street after he was elected as president on June 15, 2013, in the capital Tehran. Rowhani, the cleric who won Iran's presidential election, is a moderate who has pledged to engage more with world powers in hopes of easing crippling economic sanctions. AFP PHOTO/BEHROUZ MEHRI (Photo credit should read BEHROUZ MEHRI/AFP/Getty Images)

Watu wa jinsia zote wamefurahia ushindi wa Rouhani

Hali ya jamii nchini Iran ni mbaya kwa kweli. Ukosefu mkubwa wa ajira, ughali wa maisha unaopindukia mipaka, uchumi uliodumaa, vikwazo vikali na mengi mengine yanaonekana katika maisha ya kila siku katika nchi hiyo.

Na juu ya hayo linakuja pigo la kisiasa , ambalo lilitokana na ukandamizaji wa vuguvugu la maandamano baada ya uchaguzi wa mwaka 2009.

Hali kama hiyo ikiendelea kwa muda mrefu si rahisi kuizuwia na huzaa bila shaka hali ya kutoridhika , ambayo inaakisi matokeo ya uchaguzi huu.

Je ni kura ya maoni?

Matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Iran ni kura ya kukataa kabisa mpango wa kinuklia pamoja na sera za mambo ya kigeni ya wahafidhina na wakati huo huo pigo kwa kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei.

Iranian moderate presidential candidate, Hassan Rowhani casts his vote at a polling station in Tehran on June 14, 2013 during the first round of the presidential election. Iranians are voting to choose a new president in an election the reformists hope their sole candidate will win in the face of divided conservative ranks, four years after the disputed re-election of Mahmoud Ahmadinejad. AFP PHOTO/ATTA KENARE (Photo credit should read ATTA KENARE/AFP/Getty Images)

Rais mteule wa Iran Hassan Rowhani

Ndio sababu Hassan Ruhani katika muda wa chini ya wiki moja amekuwa mtu anayebeba matumaini ya wananchi wa nchi hiyo, katika kipindi hiki ambacho wananchi wamepoteza matumaini. Tangu siku ya kwanza anakabiliana na changamoto kubwa .

Anatakiwa kwa haraka kutafuta njia ya kuondoka kutoka katika mkwamo wa mazungumzo ya kinuklia, atafute muafaka na kubadilisha sera ambazo hazina tija na za kuchochea mambo. Ni kwa njia hiyo tu anaweza kuwa na matumaini ya kuupooza mzozo huo , ili kuweza kulegezwa vikwazo na pia kuifanya hali ya kijamii kuwa bora nchini mwake.

Kwa upande mwingine analazimika kuongoza upatanishi na jamii. Hali hiyo inawezekana tu , iwapo hatua za ukandamizaji dhidi ya jamii zitasitishwa, wafungwa wa kisiasa wataachiwa huru , hatua za kuwekwa kifungo cha nyumbani kwa mwanamageuzi Mussawi pamoja na Karoubi zitaondolewa , na mbali ya hayo uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uzuwiaji upatikanaji wa taarifa utaondolewa.

Iran's Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei casts his ballot at his office during the Iranian presidential election in central Tehran June 14, 2013. Iranians voted for a new president on Friday urged by Khamenei to turn out in force to discredit suggestions by arch foe the United States that the election would be unfair. REUTERS/Fars News/Hassan Mousavi (IRAN - Tags: POLITICS ELECTIONS TPX IMAGES OF THE DAY) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS

Kiongozi wa kidini wa Iran Ajatollah Ali Khamenei

Bila shaka kwa kuchaguliwa Ruhani matarajio ni makubwa. Mbali ya kwamba tunatambua kuwa njia ya malengo hayo ni yenye mteremko mkubwa na yenye vikwazo vingi. Kwa upande mmoja kiongozi wa kidini , kuhusiana na masuala muhimu kama suala la kinuklia , ana usemi mkubwa. Kwa upande mwingine wahafidhina katika bunge wana nguvu kubwa.

Kwa hiyo ushindi katika uchaguzi wa rais ni hatua ya kwanza. Matumaini makubwa yanaweza kuelekeza katika kuvunjwa moyo kukubwa, watu wa Iran hilo wamekwisha kuliona mara kwa mara. Lakini mara hii, wakati ni mfupi mno na gharama za kuvunjika tena moyo ziko juu mno.

Mwandishi: Jamsheed Faroughi / ZR /Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com