1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kauli ya rais Tshisekedi yazusha mvutano DRC

Saleh Mwanamilongo23 Januari 2020

Tamko la rais Felix Tshisekedi alilolitoa wakati wa ziara yake mjini London kwamba atalivunja bunge, limezusha malumbano makubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Spika wa Bunge Jeannine Mabunda amesema matamshi hayo ya rais ni kinyume na katiba huku wabunge wa chama cha rais Tshisekedi wamemtaka spika kuomba msamaha kutokana na kauli yake wanayosema kuwa inamkashifu rais.

https://p.dw.com/p/3Wh0b