1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kauli ya Museveni juu ya ukatili wa polisi yaibua hisia

Lubega Emmanuel16 Agosti 2021

Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda ya kuvishutumu vitendo vya mateso vinavyofanywa na vyombo mbalimbali vya usalama yamepolekewa kwa maoni mseto kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Kiongozi huyo ambaye amekemea vikali ukatili dhidi ya raia unaofanywa na baadhi ya maafisa wa usalama amesema utawala wake hauhusiki na mauaji ya kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/3z2Zk