1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer asema hapana haja ya kuishinikiza Ujerumani.

14 Septemba 2007

Katibu Mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa NATO Jaap de Hoop Scheffer amesema hakuna shinikizo lolote kwa Ujerumani kuweka majeshi kusini mwa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/CB1G
Katibu Mkuu wa NATO de Hoop Scheffer na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Katibu Mkuu wa NATO de Hoop Scheffer na Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: AP

Jaap de Hoop Scheffer amesema hayo mjini Berlin baada ya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier.

Baada ya mazungumzo yake na waziri Steinmeier katibu mkuu huyo wa Nato aliwaambia waandishi habari kwamba hakuna shinikizo kwa Ujerumani kupanuza shughuli zake za kijeshi nchini Afghanistan kwa kuweka askari wake kusini mwa nchi hiyo ambayo ni sehemu hatari.

Hatahivyo amesema anapandelea kuona vizingiti vichache kutoka kwa nchi wanachama inapuhusu kutumiwa kwa majeshi yao.

Madola menginne ya NATO ikiwa pamoja na Marekani, na Canada yanataka nchi zingine za mfungamano huo ziondoe vizingiti kuhusu wapi majeshi ya nchi zao yanaweza kutumika.

Lakini Ujerumani imesema kuwa itaendelea kutimiza jukumu lake la kulinda amani kaskazini mwa Afghanistan.

AM.