Kashfa zaibuliwa upya dhidi ya Zuma | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 29.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Kashfa zaibuliwa upya dhidi ya Zuma

---

JOHANNESBERG

Wafuasi wa kiongozi mpya wa chama cha African National Congress ANC nchini Afrika Kusini,Jacob Zuma wamelalamika kwamba mashtaka mapya ya rushwa dhidi ya kiongozi huyo ni sehemu ya njama ya kisiasa iliyopagwa.

Waendesha mashtaka wamemfungulia bwana Zuma mashitaka mapya ikiwa ni pamoja na uvushaji fedha na ukwepaji kodi,mbali na yale ya rushwa na udanganyifu.Afisi ya mshtaki mkuu wa serikali nchini humo imekuwa ikifanya uchunguzi juu ya tuhuma kwamba Zuma alipokea hongo na kuhusika katika kashfa nyingine zinazohusina na biashara ya silaha.Wiki iliyopita bwana Zuma alinyakua ushindi wa kukiongoza chama tawala ANC dhidi ya rais Thabo Mbeki .

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com