KARLSRUHE. Njama za kulipua ndege ya abiria zagunduliwa nchini Ujeruman i | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARLSRUHE. Njama za kulipua ndege ya abiria zagunduliwa nchini Ujeruman i

Maafisa wa usalama nchini Ujerumani wamesema kwamba wamegundua njama za kutaka kulipua ndege ya abiria hapa nchini Ujerumani.

Afisi ya muongoza mashtaka mkuu mjini Karlsruhe imeanza uchunguzi dhidi ya watuhumiwa kadhaa wanaoshukiwa kuhusika na njama hiyo ikiwa ni pamoja na kujaribu kuingiza kwa siri vifaa vya kulipuka ndani ya ndege hiyo.

Inaaminika kwamba watuhumiwa hao walifanikiwa kupitisha vifaa hivyo kwa usaidizi wa mtu aliye na uwezo unaohusu maswala ya ulinzi katika uwanja wa ndege.

Polisi wamefanya msako katika nyumba kadhaa kwenye maeneo ya makaazi ya Hessen na Rheinland Pfalz.

Wakati huo huo polisi imearifu kwamba mvulana mwenye umri wa miaka 18 aliyevamia shule moja ya sekondari katika mji wa Emsdetten karibu na mpaka wa Holand ameuwawa.

Maiti ya mvulana huyo amabe inaaminika alikuwa mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo ilikuwa na vifaa vya kujilipua.

Katika mkasa huo mwalimu na wanafunzi kadhaa wa shule hiyo walijeruhiwa.

Dahamira ya uvamizi huo bado haijajulikana na polisi wanaendelea na uchunguzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com