KARLSRUHE: Mshtakiwa wa mashambulio ya Septemba 11 awasilisha malamiko mahakamani | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARLSRUHE: Mshtakiwa wa mashambulio ya Septemba 11 awasilisha malamiko mahakamani

Mwanamume wa kwanza kushtakiwa kwa kuhusika katika mashambulio ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka wa 2001 nchini Marekani, amdwasilisha malalamiko yake kwa mahakama kuu ya Ujerumani dhidi ya hukumu yake.

Wakili wa raia wa Moroko, Mounir al Motassadeq, anayezuiliwa katika gereza moja mjini Hamburg kaskazini mwa Ujerumani, amewasilisha kesi yake kwa mahakama ya katiba ya Ujerumani mjini Karlsruhe.

Mwezi uliopita mahakama ya mjini Hamburg ilimuhukumu Motassadeq kwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na kuwa chombo cha mauaji. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mwezi ujao kuiangalia upya hukumu ya miaka saba dhidi ya mmoroko huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com