1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Ufisadi Shuleni

Grace Kabogo
20 Machi 2018

Mwalimu mkuu wa shule ya Jomvu, Bibi Gongo, anaanguka mbele ya walimu wenzake, wazazi na wanafunzi wakati wa hafla maalum ya Siku ya Wazazi na anapoteza fahamu.

https://p.dw.com/p/2lCcf
DW Crime Fighters Teil 3 School of Graft

Polisi hatimaye wanagundua kuwa aliwekewa sumu. Lakini kwa nini? Je ni kwa sababu ya walimu wenzake wenye wivu waliokitaka cheo chake? Au mtu ambaye hakukubaliana naye kuhusu kampeni yake ya kupinga rushwa kwenye shule hiyo? Inspekta Upide anapeleleza, lakini anapata mafanikio kidogo. Awa, mwalimu kijana aliyeko katika mafunzo shuleni hapo, anaanza kutafuta vidokezo yeye mwenyewe. Kidogo kidogo, anagundua kwamba kilichotokea kwa Bibi Gongo huenda kinatokana na mpango wake wa siri katika shule hiyo-kufichua dhulma za unyanyasaji wa kimapenzi dhidi ya wanafunzi unaofanywa na walimu ambao wanawaahidi kuwapa maksi nzuri.