Karandinga pia inapatikana katika Podcast | Karandinga | DW | 02.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Karandinga

Karandinga pia inapatikana katika Podcast

Michezo ya Karandinga inatoa maarifa na taarifa katika mfumo wa kuburudisha. Katika podcast hizi unaweza kusikiliza michezo ya DW kuhusu uhalifu.

Learning by Ear - Computer and the Internet - Closing the digital divide (CORBIS)

Unaweza kusikiliza michezo mipya ya Bonyeza Kiunganishi, Unaniua Taratibu, Jinamizi la Mauaji na Chozi la Mnyonge. Pia utaweza kusikiliza michezo iliyopita ya Chimbuko la Itikadi Kali, Uwindaji Haramu, Unyakuzi wa Ardhi ya chongwe na Dawa za Kutibu, Dawa za Kuuwa.

Waandishi wa Kiafrika wanaandika hadithi za kusisimua ambazo waigizaji kutoka bara lote la Afrika wanazileta katika uhalisia na kuzipa uhai. Kila hadithi kati ya hadithi nne ina vipindi kumi vyenye urefu wa dakika 12.

Hadithi ya ''Bonyeza Kiunganishi'', imeandikwa na Wanjiku Mwaurah kutoka Kenya. ''Chozi la Mnyonge'', umeandikwa na Pinado Abdu Waba kutoka Nigeria. Chrispin Mwakideu kutoka Kenya, ndiye aliyetunga hadithi ya ''Unaniua Taratibu''. Nayo hadithi ya ''Jinamizi la Mauaji'', imeandikwa na Hurcyle Gnonhoué kutoka Benin.

Hadithi ya "Chimbuko la Itikadi Kali" imeandikwa na Pinado Abdu Waba kutoka Nigeria. ''Wawindaji Haramu" umeandikwa na James Muhando kutoka Kenya. Chrispin Mwakideu pia kutoka Kenya, ni mtunzi wa hadithi ya "Unyakuzi wa Ardhi ya Chongwe".

Mukoma wa Ngugi naye pia akiwa kutoka Kenya, ametunga hadithi ya Dawa za Kutibu, Dawa za Kuua", huku Helon Habila kutoka Nigeria na Andrew Brown kutoka Afrika Kusini wakiwa kama washauri katika kuuandika mchezo huo.

 

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com