Karandinga: Dawa za Kutibu, Dawa za Kuua | Noa Bongo | DW | 15.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Noa Bongo

Karandinga: Dawa za Kutibu, Dawa za Kuua

Peter, kijana kutoka familia tajiri anakufa kutokana na kiwango kikubwa mno cha dawa. Wakati uchunguzi unapobaini hakujiua bali aliwekewa sumu, maafisa watatu wa upelelezi wanaanza uchunguzi wao.

Hatimaye wapelelezi hao wanajiingiza katika wimbi la fitina, ulafi na machafuko. Kumtafuta muuaji wa Peter, lazima wajiingize katika ulimwengu wa dawa bandia ambako watu wanaonufaika na biashara hiyo huwatumia vibaya wagonjwa na waliopoteza matumaini. Dawa bandia huuzwa kwa bei nafuu na watu hawafahamu kuhusu kitisho cha dawa hizo kwa afya zao. Taarifa kadhaa zinawapeleka maafisa hao kwa daktari mashuhuri, mganga wa kienyeji, muuzaji dawa na mpaka kwa waziri wa afya. Kadri uchunguzi unavyoendelea, maisha ya wapelelezi hao yanatishwa zaidi ya mara moja. Hatimaye, wanafaulu kutathmini ni kwa kiwango gani Peter alijihusisha na biashara hii chafu na kwa nini alitakiwa kufa. Je nini kitafuata? Fuatilia mchezo huu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.

 

 

 

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com