1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Changamoto za Plastiki

Grace Kabogo
2 Februari 2022

Katika mji mdogo wa Songa, barani Afrika, wafanyabiashara kama Mama Rosa wanakabiliwa na changamoto za marufuku ya matumizi ya plastiki zilizowekwa na serikali na kufanya biashara zao kuwa endelevu zaidi.

https://p.dw.com/p/46P4a

Crime Figters Episode 6 Plastic Challenge
Crime Figters Episode 6 Plastic Challenge
Picha: DW

Mapambano dhidi ya taka za plastiki yanaonekana kuwa ya dharura, wakati mafuriko yanayotokana na utupaji hovyo wa taka na makosa ya wanasiasa yanayoongezeka yanawasumbua watu. Tunaungana na Mama Rosa na watoto wake Kalulu na Gammy, ambao rafiki yao Ananda ana wasiwasi kuhusu kupotea kwa baba yake. Nini kimemtokea? Hadithi hii ya kusisimua inaangazia jinsi wananchi wanavyoweza kuwataka wanasiasa kuchukua hatua na kuendeleza maoni kwa ajili ya mustakabali bora, endelevu na salama. Hadithi hii imeandikwa na James Muhando kutoka Kenya.