KARACHI:Pakistan yaionya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARACHI:Pakistan yaionya Marekani

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ameionya Marekani kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi la kigaidi la Al Qaida katika ardhi yake.

Musharraf alimwambia Seneta Richard Durbin wa Marekani aliyeko ziarani nchini humo, kuwa kuzungumza juu ya uwezekano wa Marekani kuwashambulia Al qaidsa waliyoko Pakistan hakuna faida yoyote.

Amesema kuwa ni majeshi ya nchi yake tu ndiyo yatakayobeba dhamana ya kupambana na ugaidi ndani ya ardhi yake.

Kauli hiyo ya Musharraf inakuja siku moja baada ya Rais George Bush kusema kuwa jeshi la Marekani linaweza kupepeleza na kuwashambulia viongozi wa Al qaida ndani ya Pakistan.Hata hivyo Rais Bush hakusema kama Pakistan itashauriwa mapema kabla ya hatua hiyo.

Wakati huo huo Rais Pervez Musharraf amefuta ratiba ya ziara yake nchini Afghanistan kuhudhuria mkutano muhimu na makundi ya kikabila wenye nia ya kupambana na ongezeko la harakati za wanamgambo wa kundi la Taleban.

Musharraf alimwambia Rais Hamid Karzai wa Afghanistan kwa njia ya simu ya kwamba hatoweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na majukumu ya nyumbani.

Kiasi cha viongozi 700 wa kikabila na wawakilishi wa wakaazi wa milimani mpakani na Pakistan wanatarajiwa kukutana kuzungumzia hali hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com