KARACHI:Jamii ya kimataifa yakashifu shambulio la bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARACHI:Jamii ya kimataifa yakashifu shambulio la bomu

Rais wa Pakistan Pervez Musharraf anakashifu shambulio la bomu lililosababisha vifo vya watu yapata 136 na kumkosa Waziri Mkuu wa zamani Bi Benazir Bhutto baada ya kuwasili nchini mwake.Kiongozi huyo wa zamani alirejea jana baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka 8.Mlipuko huo wa jana usiku ulilenga msafara wa Bi Bhutto saa chache baada ya kuwasili nchini humo.Kwa mujibu wa polisi shambulio hilo linashukiwa kutekelezwa na mbabe wa kivita aliye na makao yake katika eneo linalopakana na Afghanistan.Hata hivyo hakuna aliyethibitisha kutekeleza shambulio hilo.

Azhar Farooqi ni mkuu wa polisi mjini Karachi

''Tumeunda timu ya uchunguzi ya wataalam wa hali ya juu na nimeenda kwenye mahala pa tukio.Baada ya uchunguzi wa mahala pale na kulingana na ushahidi tuliopata tulithibitisha kuwa ni shambulio la kujitolea muhanga.Milipuko miwili ilitokea mmoja mmkubwa na mwengine mdogo.

Shambulio hilo lililosababisha vifo vingi huenda likaathiri mazungumzo kati ya Bu Bhutto na Rais Musharraf aliyeahidi kugawana naye madaraka ili kuunda serikali ya muungano.Viongozi wa chama cha PPP wanakutana nyumbani kwake hii leo na Bi Bhutto anatarajiwa kufanya mkutano na waandhisi wa habari baadaye.

Katika mkesha wa kuwasili kwa Bi Bhutto Afisa mmoja wa serikali za mikoa alionya kuwa taarifa za ujasusi zilieleza kuwa walipuaji 3 wa kujitolea muhanga walikuwako mjini Karachi.Uongozi wa wilaya aidha ulionya kuwa Bi Bhutto huenda akashambuliwa na Taliban au wapiganaji wa kundi la Al Qaeda.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com