1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ziarani Mongolia

Martin,Prema/zpr13 Oktoba 2011

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amewasili Mongolia baada ya kukamilisha ziara yake nchini Vietnam.

https://p.dw.com/p/RqdP
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU, l.) wird am Mittwoch (12.10.11) in Ulan Bator in der Mongolei am internationalen Flughafen Dschingis-Kahn von einer mongolischen Frau begruesst, die ihr Quark als Willkommensgeschenk ueberrreicht. Foto: Oliver Lang/dapd
Kansela Merkel akikaribishwa Ulan Bator, MongoliaPicha: dapd

Wakati wa ziara hiyo, Merkel anatazamiwa kutia saini mikataba inayohusika na malighafi atakapokutana na Rais Tsakhia Elbegdory na Waziri mkuu Sukhbaatar Barbold. Mikataba hiyo itahakikisha kuvipatia viwanda vya Ujerumani, madini yenye thamani kubwa ambayo uhitajiwa katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu ,ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengenezea simu za mkononi.

Kabla ya kuwasili Ulan Bator, Kansela Merkel alisema, Mongolia inajitahidi kuelekea kwenye demokrasia. Uchumi wa nchi hiyo kwa sehemu kubwa unategemea majirani wake Urusi na China. Merkel ni kansela wa kwanza wa Ujerumani kuizuru Mongolia nchi iliyo na wakaazi milioni tatu.