Kansela wa Ujerumani akutana na Waziri Mkuu wa Lebanon | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Kansela wa Ujerumani akutana na Waziri Mkuu wa Lebanon

BERLIN:

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekutana na Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora mjini Berlin.Merkel ameunga mkono jitahada za upatanisho za Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusika na kuteuliwa kwa rais wa Lebanon ili kuziba pengo la uongozi nchini humo.Kuambatana na mpango mpya wa maafikiano,wadhifa wa urais unatazamiwa kwenda kwa mgombea Michel Suleiman ambae hivi sasa ni mkuu wa majeshi.

Merkel amekariri kuwa Ujerumani itasaidia kujenga upya utaratibu wa kidemokrasia nchini Lebanon.Wakati huo huo akatoa mwito kwa Syria kuchukua hatua zitakazosaidia kutenzua mzozo wa Lebanon.Upande wa upinzani nchini Lebanon unaoongozwa na chama cha Hezbollah cha Washia wenye itikadi kali,unaungwa mkono na Syria.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com