Kansela wa Austria ziarani Ujerumani | Magazetini | DW | 18.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Kansela wa Austria ziarani Ujerumani

Wahariri wa magazeti Ujerumani wamejishughulisha  na ziara ya kansela wa Austria Sebastian Kurz nchini Ujerumani, uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano mkuu, na hatua ya Marekani kupunguza mchango wake kwa UNRWA.

Berlin Sebastian Kurz, Österreich & Angela Merkel, Deutschland (Reuters/F. Bensch)

Kansela wa Austria Sebastian Kurz (kushoto) na kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Tukianza  na  mada  kuhusu  ziara  ya  kansela  wa Austria nchini Ujerumani , mhariri  wa  gazeti  la  Berliner Zeitung  anaandika.

Muungano wa serikali  wa rangi  nyeusi  na  buluu kama unavyoitwa nchini  Austria  hadi sasa  ni  wa  aina  ya mfano  barani  Ulaya, ambapo  vyama  vya  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  vimepata mafanikio  makubwa  kila  mahali  na  kwamba  wakati  huu  ama baadaye  vitaweza  kuwa  sehemu  ya  serikali. Gharama ya mafanikio  haya, lakini  ni  kwamba  kansela  Sebastian Kurz anaweza  kukibana  chama ambacho  hakipendi wahamiaji  katika Ulaya  cha  FPO. Na  hili  pia  lina matatizo  yake, na  huenda  hivi karibuni  yakaonekana, hususan wakati  Austria  itakapochukua uongozi wa  Umoja  wa  Ulaya  katikati  ya  mwaka  huu. Miongo kadhaa  ya  kuwa  na  mahusiano  ya  karibu  na  Ujerumani  imepita. Kansela  Kurz  wa  Austria  anatafuta  sasa  washirika  wapya katika  Ulaya.

Kuhusu  mada  hiyo  hiyo Gazeti  la  Badische Neueste Nachrichten la  mjini  Karlsruhe  linaandika:

Kansela  Angela  Merkel  mwenye  matatizo  hawezi  kufurahia , kwamba  kijana  kutoka  mjini  Vienna  atakuwa  ni  mada  ya kujadiliwa  hapo baadaye. Hususan  katika  suala  la  sera  za wakimbizi, suala  ambalo  kansela  Kurz tayari  kama  waziri  wa mambo  ya  kigeni analidhihirisha, na  ni  suala  ambalo  litahitaji kuidhinishwa.  Na  hata  katika  kiwango  cha  Ulaya  itabidi kupambana  na  kansela  Kurz , kwa  kuwa  madai  yake, hayaishii  tu katika  mipaka  ya  taifa  hilo  la  Austria.

Gazeti  la  Ludwigsburger Kreiszeitung  likizungumzia  kuhusu mazungumzo  ya  kuunda  serikali  ya  mseto  kati  ya  chama  cha CDU / CSU  na  SPD  linaandika.

Muhimu  zaidi  ni  kwamba,  mapitio  ya  hivi  sasa  kwa  pande  zote mbili yana  uwezekano  mkubwa, kwamba hali  bora  ya  muungano inaweza  kufikia  mwisho  na  kuiingiza  nchi  katika  mkwamo mkubwa. Iwapo  hali  kama  hiyo  ya  dharura  itatokea.  Bila  ya upande  mmoja  kusababisha  vurumai , iwapo kutatokea  hali  ya kuvunjika  kwa  muungano  huo. Makubaliano  hususan kwa  upande wa  SPD  yanaelekea  vizuri , na  hali  ya  tahadhari  inapaswa  pia kuwapo, na  sio  upande  wa  chama  cha  kansela  Merkel kuwawekea  mbinyo  zaidi. Mradi  huu  pia  unapaswa  kuwa muafaka  kwa  wapinzani  wengi  wasipendelea  vyama  hivyo kuunda  serikali. Pamoja  na  hayo  kansela  Merkel  pia  anaweza kutumia   matokeo ya muda  huu  kutumia  busara kujiondoa.

Nae mhariri  wa  gazeti  la  Rhine-Neckar - Zeitung   kuhusiana  na mada  hiyo  anaandika:

Ni mapema  mno  kuikumbusha  serikali  mpya  ya  chama  cha CDU/CSU  na  SPD kuhusu  mazungumzo ya  viwango  vya mishahara. Ni  kama  muziki  ambao  unaelekea  kufikia  mwisho. Kwa  kweli  kunaonekana  kuwapo  na  hali  ya  wasi  wasi,  iwapo serikali  kama  hiyo  inaweza  kutokea. Kwa sababu  hali  ya  mjadala wa muungano  wa  serikali  kati  ya  chama  cha  CDU  na  SPD haupigi  hatua.

Mada  ya  mwisho  ni  kuhusu Marekani  ilivyochukua  hatua  ya punguza  mchango  wake  katika  shirika  la  kuwahudumia  wakimbizi wa  Kipalestina  UNRWA. Gazeti  la  Nordwest-Zeitung  la  mjini Oldenburg linandika:

Katika  mataifa  ya  Kiarabu  hivi  sasa  kuna  ukimya  kuhusiana  na hali  ya  wakimbizi  wa  Kipalestina. Katika  Ukanda  wa  Gaza  na ukingo  wa  magharibi  shirika  la  UNRWA  ndio  linashughulikia matatizo  ya  wakimbizi  wa  Kipalestina.  Shirika  hili  la  Umoja  wa Mataifa  linawajibika  kuwahudumia  wakimbizi  wa  vizazi  na  vizazi. Zaidi  ya  hayo  katika  Ukanda  wa  Gaza  UNRWA  linawapatia  kazi maelfu  ya  watu  wanaounga  mkono  kundi  la  Hamas. Katika  shule zinazohudumiwa  na  shirika  hilo  wanajitokeza  wafuasi  wa  kundi hilo  ambao  wanachochea  chuki  dhidi  ya  Israel. Kwa  ujumla mhariri  anaandika  kwa   shirika  hilo  ni  sehemu  ya  matatizo na sio  suluhisho.  Ni  vizuri  kulitaja  tatizo  kwa  jina  lake.

Kwa maoni  hayo  ndio  tunafikia  mwisho  wa  kuwaletea uchambuzi wa  yale  yaliyoandikwa  na  wahariri  wa  magazeti  hapa  Ujerumani , kama  mlivyokusanyiwa  na  Sekione  Kitojo.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Gakuba, Daniel